Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni mwa Taasisi zinazonufaika na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET) ambapo hii leo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha ameongoza Menejimenti ya Chuo na Waratibu wa Mradi wa HEET katika hafla ya kutia saini Mkataba wa ujenzi wa majengo ya TEHAMA na Taaluma Kampasi Kuu Morogoro.

Amesema, Chuo Kikuu cha Mzumbe kilipokea fedha kutoka Benki ya Dunia kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 21 kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu Mipya katika Chuo Kikuu cha Mzumbe (Kampasi Kuu na Kampasi ya Tanga).

Miongoni mwa fedha zilizotengwa TZS. 17,574,178,385.37 zitatumika kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu Mipya katika Kampasi Kuu Morogoro. Mkataba huo ni kati ya Chuo Kikuu Mzumbe na Mkandarasi Shanxi Construction Investment Group Co. Ltd kwa gharama ya Bilioni13.3.

Prof. Mwegoha ametaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anazingatia matakwa ya Mkataba kwa kukamilisha jengo kwa wakati na kuzingatia ubora wa hali ya juu.

Awali Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri Prof. Eliza Mwakasangula amesema Jengo la taaluma litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyakazi 100, madarasa na kumbi za mihadhara zitakakazochukua wanafunzi 1000 kwa wakati mmoja. Aidha, jengo la TEHAMA litakuwa na kumbi za mikutano na maabara za mafunzo kwa ajili ya bunifu mbalimbali.

Kwa upande mwingine Msimamizi wa Mradi kutoka Kampuni ya Shanxi Contruction Investment Group Co. Ltd. Mhandisi William Zhang amesema wako tayari kuanza kazi mara moja na kuahidi kukamisha kwa wakati

Ujenzi wa majengo haya unatarajia kuchukua miezi kumi na nannie na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 13.3 na unajengwa na Mkandarasi Shanxi Construction Investment Group Co. Ltd kutoka China.

*****

 

 

 

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top