Waratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe wamefanya Kikao na Wakaguzi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Allen Mushi amewakaribisha wakaguzi hao wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoloji na kusema Chuo Kikuu Mzumbe kitawapa ushirikiano katika kazi za ukaguzi ili kupata nyaraka zote zitakazohitajika na kupata ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayofanyika katika mradi.
 
Mkaguzi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Fidel Rwehumbiza amesema "Ukaguzi huu ni shirikishi na tunategemea kushauriana tufanye nini pale eneo linapokuwa linaenda taratibu."Pia, Waratibu hao watembelea Wilaya ya Mkinga eneo ambalo Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Tanga kitajengwa na kuona kiasi gani wenyeji wa eneo hilo wanajua nini kinaendelea kwenye vijiji na wilaya zao.
 
Pamoja na hilo, Wakaguzi hao kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wameambatana na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa ndani wa serikali ili kushirikiana katika zoezi hilo. Naye, Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Hawa Tundui amewashukuru Wakaguzi hao na kuahidi kuwa Waratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe watawapa ushirikiano wa karibu katika kukamilisha kazi yao.
 
*****************************************

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top