Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha leo Februari 6, 2024 ameongoza mjadala katika Kikao Kazi cha 4 cha Serikali Mtandao kuhusu usimamizi madhubuti wa masuala ya Serikali Mtandao.
Katika mjadala huo, mada tatu ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na tathmini ya utekelezaji wa Serikali mtandao, uzingatiaji wa sheria ya mtandao ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020, mtangamano na kubadilishana taarifa.
 
Mada nyingine iliyojadiliwa ni mpango mkakati wa Serikali Mtandao na ulinzi wa makosa ya kimtandao.
Prof. Mwegoha ametoa rai kwa washiriki wa mkutano huo kupenda kujielimisha na kujenga uwezo wa ndani katika kuhakikisha uzingatiaji wa sheria ya mtandao na uzuiaji wa makosa ya kimtandao unapewa kipaumbele serikalini.
Mkutano wa 4 wa Mamlaka ya Serikali Mtandao unafanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 6-8 Februari, 2023 na washiriki ni pamoja na Maafisa Masuuli, Wakuu wa Idara na Vitengo vya TEHAMA, Wasimamizi wa Mifumo na Maafisa Habari.

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top