Makamu mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha amewaongoza wajumbe wa Menejimenti kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Ndaki ya Mbeya.
 
Miradi iliyokaguliwa na kutembelewa ni pamoja na mradi wa upanuzi wa jengo la zahanati ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 75%, mradi wa ukarabati wa viwanja vya michezo hasa mchezo wa kikapu ambao pia umefikia asilimia 60% na mradi wa ukarabati wa jengo la Hosteli ya Borito.
 
Akitoa ufafanuzi Mhandisi Ndipie Tilon amesema utekelezaji wa miradi hiyo iko katika hatua za mwisho za ukamilishaji na kuwahakikishia wajumbe wa Menejimenti pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo kwamba miradi hiyo itakamilika kwa wakati na kuzingatia viwango vya ubora vilivyokubalika kwa mujibu wa mkataba.
 
"Kwa sasa tupo hatua za mwisho kukamilisha miradi hii, hivyo niwahakikishie Menejimenti na Makamu Mkuu wa Chuo kazi inakwenda kukamilika hivi karibuni" amesisitiza Mhandisi Ndipie.
 
Prof. Mwegoha pamoja na Menejimenti wamemtaka Mkandarasi kuhakikisha kuwa miradi hii inakamilika kwa wakati kama walivyo kubaliana.
 
*********
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top