Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, ametembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kukaimu nafasi hiyo.

Prof.Mwegoha, ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo, na kusisitiza watumishi wanaotekeleza miradi hiyo kuongeza kasi na  kuzingatia utaalamu, ikiwa ni pamoja na kutumia fedha kulingana na bajeti iliyoidhinishwa ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa.

Katika ziara hiyo kaimu Makamu Mkuu wa chuo aliambatana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala,  Prof. Allen Mushi, Wajumbe wa Menejimenti na wataalamu wa Kitengo cha miliki na majengo wenye dhamana ya kusimamia miradi hiyo.

**************************

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (wa nne Kushoto) akijadiliana na wataalamu mara baada ya kukagua ukarabati wa jengo la kusomea kwa wanafaunzi wa Shahada ya uzamivu (PhD).

Prof. William Mwegoha, akitazama ukarabati unaoendelea katika jengo la Maktaba Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu Morogoro.

Prof. Mwegoha akikagua maandalizi yanayofanyika eneo litakapojengwa jengo jipya la Utawala katika eneo la Maekani Kampasi Kuu Morogoro. Mradi huo utaanza utekelezaji hivi karibuni.

Ukaguzi ukiendelea wa maandalizi ya eneo yatakapofanyika Mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe  kampasi  Kuu Morogoro.

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: mu@mzumbe.ac.tz
Go to top