Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe.Albinus Mgonya, leo Machi 24 amekabidhi kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.John Joseph Pombe Magufuli kwa Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe ikiwa ni ishara ya kuwa maombolezo hayo yanafanyika rasmi kiwilaya katika Taasisi hiyo ya elimu ya juu

Akikabidhi kitabu cha maombolezo Mhe.Mgonya amesema kuwa kitabu hicho kitazunguka katika Taasisi zote zilizopo wilaya ya Mvomero kwa kipindi cha siku 21 za maombolezo na kwamba Chuo Kikuu Mzumbe ndiyo taasisi inayozindua utaratibu huo ambapo kitabu kitakaa chuoni hapo kwa muda wa siku tatu mfululizo ikiwemo siku ya mazishi.

Mhe.Mgonya amesema Hayati Dkt.John Pombe Magufuli alikuwa ni Kiongozi Mzalendo,Mchapakazi,Mwadilifu na aliyependa sana nchi yake na kwamba Watanzania wote tunao wajibu wa kuyaenzi na kuyatekeleza mema yote aliyotuachia.

Akipokea kitabu hicho Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Ganka Nyamsogoro,amesema Chuo Kikuu Mzumbe kimepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa Hayati Dkt.Magufuli na kueleza katika muda mfupi aliohudumu alifanya uwekezaji mkubwa sana katika miradi ya maendeleo ikiwemo Sekta ya elimu na kwamba Chuo kikuu Mzumbe ni miongoni mwa Taasisi zilizonufaika na uwekezaji wake kwani kiliwezeshwa shilingi bilioni 6.5 kwa ajili ya kujenga hosteli zenye uwezo wa kuchukua Wanafunzi 1024 kwa mara moja

Prof Nyamsogo aliongeza kuwa Chuo kimepokea kwa heshima kubwa kitabu hicho cha maombolezo cha wilaya  na kwamba Wanajumuiya wa Chuo  Kikuu Mzumbe watazitumia vyema siku tatu za kusaini kitabu, kwani wanautambua vyema mchango mkubwa uliotolewa na Hayati Dkt.Magufuli

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe.Albinus Mgonya (Mwenye suti nyeusi) akiwa ameambatana na ujumbe wake wakiwasili Chuo Kikuu Mzumbe

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Ganka Nyamsogoro akiweka shada la maua katika picha ya Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli baada ya kuwasili kwa kitabu cha maombolezo chuoni hapa.

Baadhi ya Wanachuo wakiwa katika foleni ya kusubiri kusaini kitabu cha maombolezo

MWanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe akisaini kitabu cha maombolezo baada ya kumaliza  Mtihani Inayoendelea ya Kumaliza mhura.

MWanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe akisaini kitabu cha maombolezo baada ya kumaliza  Mtihani Inayoendelea ya Kumaliza mhura.

 

 

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: mu@mzumbe.ac.tz
Go to top