Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Ali Mohamed Shein, amesimikwa rasmi kuwa Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe na kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu Mhe.Barnabas Samatta ambaye amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 12 kuanzia Januari 2009 na muda wake ulifikia tamati tarehe 2 Januari,2021 .

Akihutubia katika hafla ya kusimikwa kwake iliyofanyika tarehe 5 Januari,2021 katika viwanja vya Mahafali, Kampasi kuu Morogoro, Mhe.Dkt.Shein ameahidi kukiunganisha Chuo kikuu Mzumbe na vyuo vikuu vya ndani na nje ya nchi ili kuendeleza Tafiti ,Taaluma na maendeleo yote yaliyokwishaanzishwa na Mtangulizi wake.

Baada ya hafla ya kusimikwa Mhe.Dkt.Shein, alitembelea miradi ya ujenzi wa hosteli na madarasa iliyopo eneo la Maekani ambapo alifurahishwa na ujenzi madhubuti na ubora wa miradi hiyo zikiwemo samani ambazo zimewekwa katika madarasa.

Hafla ya kusimikwa Mhe.Dkt.Shein ilihudhudhuriwa na Viongozi  wa Serikali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Wizara ya Muungano na Mazingira) ,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia, ,Makamu Wakuu wa vyuo akiwemo  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar  (SUZA),Makamu wakuu wa Chuo kikuu Mzumbe waliopita,Taasis na Wadau wa elimu ya juu, uongozi wa mkoa wa Morogoro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, uongozi wa Wilaya ya Mvomero wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya,Taasisi jirani,Wafanyakazi,Wanafunzi na Wananchi  wanaoishi karibu na Chuo Kikuu Mzumbe.

***********************************************************

 

 

PICHA:Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt Ali Mohamed Shein (aliyevaa suti nyeusi) akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu Mstaafu wa fedha za Serikali, CPA.Ludovic Uttoh mara baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe kwa ajili ya hafla ya kusimikwa kwakwe.

PICHA:Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt Ali Mohamed Shein akivishwa vazi rasmi (joho na kofia) ikiwa ni ishara ya kusimikwa kwake.Wanaomvika kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, CPA Pius Maneno na kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe Prof.Lughano Kusiluka.

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: mu@mzumbe.ac.tz
Go to top