Chuo Kikuu Mzumbe kimepongezwa kwa umahiri wake katika ufundishaji masomo ya sheria, na kuwa Chuo bora chenye wahitimu mahiri na wajuzi kwenye fani ya Sheria nchini.  

Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipotembelea Chuo hicho kwa mara ya kwanza, tangu ameteuliwa kushika nafasi hiyo; akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Prof. Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju na baadhi ya watendaji kutoka taasisi na Idara za Sheria zilizopo chini ya Wizara hiyo.

Pamoja na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe, amewataka kuongeza ubunifu zaidi katika kutoa wanafunzi bora, kwa kuzingatia miiko ya kazi ili kuwaandaa vijana wenye nidhamu na weledi.

Chuo Kikuu Mzumbe ni Chuo cha Umma kinachotoa kozi mbalimbali za Sheria kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma), Shahada ya Awali (Degree) na Shahada za Umahiri (Masters) katika Sheria.

 

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akitoa taarifa kwa Waziri kuhusu maendeleo ya Chuo

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi.Dkt.Augustine Mahiga akizungumza na wanataaluma wa Kitivo cha Sheria wa Chuo Kikuu Mzumbe

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo ya awali ya lengo la ziara

Wataalamu wa kitivo cha Sheria wakimsikiliza Waziri

 

Waziri akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wahadhiri wa Sheria Chuo kikuu Mzumbe.

 

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top