CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kimetoa mafunzo kwa wataalam na wanafunzi kada ya rasilimali watu ili kuwaongezea uwezo katika kukabiliana na ushindani kwenye soko. 

Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maafisa rasilimali watu (Human Resource Association of Tanzania (HRSTA), yamelenga kuwawezesha wataalamu kuijitambua na kuonesha taswira au muonekano stahiki kwa jamii kulingana na malengo yao ya kimaisha.   

 Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa Chuo cha Mzumbe  Kampasi ya Dar es Salaam Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi amesema kuwa chuo kimeona umuhimu wa wataalamu wanaozalishwa chuoni  kujitofautisha kutoka katika makundi ya watu wengi kwa kuwa na vitu vya kipekee au ubunifu kwenye soko.

“Ukijitengeneza wewe mwenyewe na kuwa tofauti kwenye soko basi hupati shida ya kujieleza sana kwenye soko” alisisitiza Prof. Ngowi.

 Kwa upande wake, Mratibu wa Jumuiya ya Maafisa rasilimali watu (Human Resource Association of Tanzania (HRSTA), Bw Emmanuel Mnyawami, amesisitiza kuwa kwa sasa dunia ina ushindani sana katika kila taaluma, hivyo ni lazima mtu binafsi afanyejitihada kubwa ili aonekane katika soko.

 “Mafunzo haya yanalenga kuwapa uwezo maafisa rasilimali watu na wanafunzi wa fani hiyo waweze kufanya  uonekane” Bw. Mnyawami amesema.

 Akifafanua kuhusu kuendesha mafunzo hayo hapo chuoni, Mkuu wa Idara ya Kozi Fupi na Huduma za Shauri za Kitaaluma, Dkt. Faisal Issa amesema mafunzo hayo yamefanyika kwa mara ya tatu sasa yakiwa na lengo ni kutanisha wanachuo na wanajumuiya wa jumuiya ya Maafisa Rasilimali watu(HRSTA) ili kupata uzoefu katika taaluma hiyo. Mtoa mada mkuu alikuwa ni Bw. Carl Bosser ambaye ni mshauri mwelekezi.

Bw. Carl Bosser ambaye ni mshauri mwelekezi akitoa mada kuhusu "Personal Branding.

Mkuu wa  Kampasi ya Dar es Salaam Profesa  Prosper Honest Ngowi akisisitiza jambo  alipokuwa akifunga mafunzo ya siku moja ya wataalam na wanafunzi kada ya rasilimali watu yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maafisa Rasilimali Watu Tanzania (Human Resource Association of Tanzania (HRSTA).

Mkuu wa Kampasi Prof. Prosper  Honest Ngowi (katikati), Mkuu wa Idara ya Kozi Fupi na Huduma za Shauri za Kitaaluma, Dkt. Faisal Issa ( kushoto) pamoja na wanafunzi wa Shahada ya Uzamili  katika masoko Yusuphu Zuberi wakifuatilia mada pamoja na washiriki wengine.

 

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top