Chuo Kikuu Mzumbe kimeshiriki kwa mara nyingine Mkutano wa saba (7) wa Mpango wa Mafunzo kwa Nchi za Maziwa Makuu katika masuala la Kimataifa ya Sheria za Kibinadamu na Haki za Binadamu; uliofanyika katika mji wa Kigali nchini Rwanda. Katika Mkutano huo Chuo Kikuu Mzumbe kimeibuka mshindi wa nne katika shindano la Mahakama ya kufundishia (Moot court) ambapo wanafunzi kutoka jumla ya Vyuo Vikuu 30 katika Ukanda wa Afrika vilishiriki, vikiwemo vyuo vingine vikuu vya Tanzania. Nchi ya kwanza ilikuwa Kenya, ikifuatiwa na Uganda. Mzumbe iling’ara katika mkutano huo baada ya kuchukua zawadi nyingine ya kikombe kufuatia ushindi mwingine iliyopata kupitia mwanafunzi wake Bi. Hazel Karua kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Utetezi wa Hoja.

Mkutano huo umelenga kuwa na mikakati ya muda mrefu na mfupi katika kuimarisha Amani na utekelezaji wa Haki za Binadamu kwa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, kwa kutoa mafunzo na elimu inayohusu sheria za kimataifa katika masuala ya kibinadamu na Haki za Binadamu. (International Humanitarian Laws and Human Rights).

Wataalamu wabobevu katika masuala ya sheria za Kimataifa, Watetezi wa Haki za Binadamu kutoka Umoja wa Afrika, wataalamu wa masuala ya Wakimbizi na Watetezi wa haki za wazawa Afrika walipata fursa ya kuwasilisha mada ambazo zilijadiliwa.

Chuo Kikuu Mzumbe kiliwakilishwa na Mhadhiri Deogratius Mapendo kutoka Kitivo cha Sheria, pamoja na wanafunzi Jeofrey Ernest Lukwaro  na Bi. Hazel Karua wote wa mwaka wa tatu kozi ya Sheria inayotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe.

 

Baadhi ya Wanafunzi wawakilishi kutoka Tanzania wakishiriki mafunzo kuhusu Sheria za kimataifa za masuala ya Kibinadamu na Haki za Binadamu, Kigali Rwanda.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mjadala kuhusu masuala la Sheria za kimataifa kuhusu masuala ya Kibinadamu na Haki za Kibinadamu ukiendelea, Kigali Rwanda.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Wakiwa kwenye picha ya pamoja, ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Bw. Deogratius Mapendo (Katikakati) pamoja na wanafunzi waliowakilisha Chuo Kikuu Mzumbe katika mashindano Bw. Jeofrey Ernest Lukwaro (kushoto) na Bi. Bi. Hazel Karua (kulia).

 

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top