Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, ameweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya; wakati wa ziara yake ya siku 9 mkoani Mbeya.

 Akuzungumza mara baada ya kuweka jiwe hilo Rais amepongeza uongozi wa Chuo hicho kwa jitihada za makusudi za kuendeleza Chuo hicho na kuahidi kuendelea kusaidia maendeleo ya chuo hicho kupitia bajeti ya Serikali upande wa Elimu.

 Mara baada ya kukagua baadhi ya sehemu za jengo hilo, Rais ameonyesha kuridhishwa na ubora wa jengo hilo na kusisitiza kukamilika kwa wakati ili kutoa fursa kuanza kutumika.

 Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Lughano Kusiluka; Jengo hilo litakuwa na vyumba ya madarasa na mikutano vyenye uwezo wa kubeba wanafunzi 900 kwa mara moja   pamoja na ofisi za Utawala kwa wafanyakazi wapatao 48.

PICHA YA JUU: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la Msingi ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Profesa  Joyce Ndalichako, akifuatiwa na Profesa Lughano Kusiluka Makamu Mkuu wa Chuo hicho, nawa mwisho kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila. Anayeshuhudia kwa karibu tukio hilo kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Matthew Luhanga.

Makamu Mku wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka akiwa ameshikana mkono na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akitoa maelezo kuhusu hatua za ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala.

Rais Magufuli akipokea maelezo ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka (kushoto), baada ya kumaliza uwekaji jiwe la msingi la chuo hicho na kukagua hatua za ujenzi.

 Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya lilowekewa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

 

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top