Chuo Kikuu Mzumbe kina mpango wa kuanzisha kituo kikubwa cha kulea na kukuza wajasiriamali ili kukuza vipaji na mawazo mbalimbali biashara ya kibunifu kutoka kwa Wanajumuiya ya Chuo na nje ya Chuo.  

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka katika hotuba yake ya ukaribisho kwa Mh. Hussein Bashe Mbunge wa Nzega na Mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe. 

Mheshimiwa Bashe ametembelea Chuo Kikuu Mzumbe na kuongea na jumuiya ya Wanafunzi katika hafla maalum ya kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa kwanza wa program mbalimbali.

 Mh Bashe akiwa ni mhitmu wa  Mzumbe , amepongeza hatua mbali mbali za maendeleo katika Chuo hiki na kuahidi kuendelea kushirikiana na Uongozi wa Chuo ili kuhakikisha ndoto ya kuwa na kituo bora na kikubwa cha kukuza wajasiriamali zinafikiwa.  Pia amemuhakikishia Makamu Mku wa Chuo Kuwa atawashirikisha wabunge waliosoma Mzumbe ili kwa pamoja kama wahitimu

 “alumni” waweze kutembelea Chuo na kushiriki katika hatua mbalimbali za maendeleo

               “ uanzishwaji wa “ incubation center ni hatua muhimu katika kuhakikisha                vijana hususan wanaohitimu hapa Mzumbe wanashiriki moja kwa moja                katika kujenga uchumi wa     viwanda , nami niahidi kuwashirikisha                wabunge wenzangu wahitimu wa Mzumbe tutembelee chuo na kushiriki                 katika  kukuza Chuo chetu”

Katika hatua nyingine Mh.Bashe amewasihi vijana kuwa na malengo tena malengo makubwa na kuhakikisha  yanafikiwa. Akizungumza na wanafunzi amewasihi kusoma wakiwa na ndoto na wahakikishe ndoto zao wanaanza kuzitekelezwa wakiwa bado ni Wanachuo. 

Mh Bashe alifurahishwa na wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza ambao ni wabunifu na wajasiriamali, waliofanya maonesho ya Bidhaa zao mbalimbali na aliwachangia kiasi cha Milioni moja kwa ajili ya kukuza mitaji yao.

 

Katika hatua nyingine Mh Bashe alifurahishwa na vipaji mbalimbali vilivyoneshwa katika sanaa, ambapo alishuhudia uimbaji, uchoraji, ulimbwende na maonesho ya sarakasi yaliyofanywa na wanafunzi hao, ambapo pia alichangia million moja kupitia Serikali ya wanafunzi (MUSO)  ili kuandaa na kuzindua Blog itayotumika kusambaza taarifa juu ya vipaji na bidhaa mbalimbali za wajasiriamali.

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top