Katika kuitikia na kuunga mkono adhma ya Serikali ya Awamu ya Tano inyoongozwa na Mheshimiwa Raisi Dkt. John Pombe Magufuli ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Tanzania, Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Skuli ya Utawala na Menejementi (Kitengo cha Sera na Uongozi) kimeandaa programu ya mafunzo juu wajibu na nafasi za Kamati za Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Mafunzo haya yamewalenga madiwani ambao in wajumbe wa kamati za fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo kila Mamlaka ya Serikali ya Mitaa inashauriwa imgharamie Meya na Makamu Meya/Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti.

Gharama za mafunzo kwa mshiriki mmoja ni Tshs 350,000/= tu ikiwa ni gharama ya ada ya mafunzo, kifungua kinywa, chakula cha mchana pamoja na makablasha ya mafunzo. Kila mshiriki atapatiwa Cheti cha ushiriki baada ya mafunzo. Mafunzo haya yamepangwa kufanyika katika kanda kuu tano kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali Namba 1 hapo chini:

Jedwali Namba 1: Mgawanyo, mahali na tarehe ya Mafunzo kikanda

NA

KANDA

MIKOA MAFUNZO YATAFANYIKA

TAREHE

UKUMBI

1

Kanda ya Ziwa

Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga na Kigoma

20-22 Juni, 2018

Chuo Kikuu Mzumbe-Kituo cha  Mwanza

2

Kanda ya Nyanda za Juu Kusini

Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Katavi, Rukwa na Songwe

25-27 Juni, 2018

Katavi

3

Kanda ya Kati

Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma

29 Juni- 2, 3 Julai 2018

VETA, Dodoma

4

Kanda ya Kaskazini

Kilimanjaro, Arusha,  Manyara na Tanga

5-7 Julai, 2018

RAS Arusha

5

 

Kanda ya Mashariki

Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Mtwara na Lindi

 9-11 Julai, 2018

Shirika la Elimu Kibaha

 Ikiwa Mamlaka ya Serikali za Mitaa inataka Madiwani wake wapatiwe mafunzo haya peke yao kwa kufuatwa mahali ilipo Mamlaka hiyo, Chuo kitatoza TZS  200,000 kwa kila mshiriki kama ada ya utaalamu (Chuo hakitahusika na gharama ya ukumbi na chakula).

Ada ya mafunzo inaombwa kuingizwa katika akaunti ya Chuo Kikuu Mzumbe, Benki ya CRDB Na. 01J1076853301. Jina la akaunti ni MU-SHORT COURSES AND CONSULTANCY baada ya kulipa fedha tafadhali wasiliana na waandaaji kwa kutuma nakala ya benki (bank sleep) katika barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.. Tarehe ya mwisho ya malipo kwa washiriki wa mafunzo haya ni siku mbili kabla ya kuanza mafunzo kwa kanda husika. Kwa taarifa zaidi pamoja na kuthibitisha ushiriki tafadhali wasiliana na Bw. Anosisye Kesale 0714005555 (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.) au Dkt. Saida Fundi 0688 557056 (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ). Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi fupi na ushauri wasiliana nasi kupitia barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

“Tujifunze kwa Maendeleo ya Watu”

Bofya hapa ku-download pdf file. 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top