Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji Mkuu Mstaafu Mh.Barnabas Samatta leo 05/02/2018 ameanza rasmi ziara ya kutembelea Vyuo Vikuu vyote vya Mzumbe kwa kuzungumza na Wafanyakazi na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu ya Morogoro sambamba na kukagua miradi ya miundombinu ya majengo katika Chuo hicho ikiwemo eneo ambalo litajengwa mradi mkubwa wa Mzumbe mpya ambapo tayari barabara zitakazounganisha eneo hilo na Mzumbe ya sasa zimeshaanza kutengenezwa ili kurahisisha ujenzi wa mradi huo mkubwa.

Katika nasaha zake Mh.Samatta amewataka Wafanyakazi na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuendeleza sifa nzuri ya Chuo hicho ambacho kwa mujibu wa Vyombo vinavyofuatilia ubora wa Vyuo duniani wamekitaja Chuo Kikuu Mzumbe kuwa katika  nafasi ya 179 kwa ubora kati ya Vyuo vikuu  1493 vilivyoshindandishwa kitaaluma barani Africa na hivyo kuwasihi kuendeleza utamaduni huo mzuri wa kutoa Taaluma bora,uadilifu,ufanisi,kulinda Uhuru wa Taaluma na pamoja na kuendelea kuzingatia usawa wa jinsia.

Ziara ya Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe itafanyika kwa siku tano na atatembelea Vyuo Vikuu vyote vya Mzumbe vilivyopo katika mkoa wa Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam kuzungungumza na Wafanyakazi,Wanafunzi pamoja na kukagua miradi  katika Vyuo vyote. 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top