WAHITIMU wa chuo kikuu Mzumbe wametakiwa kuwa wazalendo kwa kutunza na kusimamia rasilimali za umma kwa maendeleo ya Taifa. Wito huo umetolewa na Mlau wa Chuo kikuu Mzumbe Dk. Hawa Tundui alipokuwa akitoa nasaha kwa wahitimu wakati wa mahafali ya 21 ya chuo hicho.Dk. Tundui alisema kuwa uzalendo ni chachu na mtaji katika maendeleo ya nchi hivyo kutumika na kutunza vizuri rasilimali kutasaidia Taifa kuondokana na hasara zinazoweza kutokea kutokana na kutokuwa na usimamizi bora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu Mzumbe Dk. Saida Yahya Othuman alimshuku Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kushika nafasi hiyo.Dk. Saida aliahidi kukisimamia chuo hicho ili kiweze kupiga hatua katika utekelezaji wa mipango yote ya chuo hicho.Aliwataka wahitimu hao kwenda kuleta mageuzi kwenye jamii huku wakitambua kuwa mageuzi hayaji kwa kutumwa bali kwa kutumikia.

Naye kaimu makamu mkuu wa chuo kikuu Mzumbe Profesa William Mwegoha alisema kuwa jumla ya wahitimu 2631 watatunukiwa katika mahafali hayo.

*******************************************************

Sehemu ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe wakishangilia katika sherehe za mahafali ya chuo hicho yaliyohudhurishwa na Mkuu wa

Chuo Kikuu Mzumbe Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ally Mohammed Shein wakati wa mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi

Kuu Morogoro yaliyofanyika leo Novemba 24,2021 mjini Morogoro. 

 

 

 

 

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: mu@mzumbe.ac.tz
Go to top