Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka amewataka Wafanyakazi na Wanajumuiya wa chuo hicho kushiriki michezo mbalimbali inayoandaliwa Chuoni hapo kwani ni muhimu kwa afya ya akili na mwili sambamba na  utekelezaji wa Sera ya Kitaifa ya michezo.

 Prof. Lughano Kusiluka amesema hayo wakati wa bonanza la michezo lililofanyika mwishoni mwa wiki, kampasi kuu Morogoro ambalo lililenga kuchagiza utamaduni wa kushiriki michezo kwa afya ya akili na mwili kwa wafanyakazi na Wanajumuiya wa chuo hicho.

  “ Michezo ni ya wote na kwa watu wote, lengo ni kukaa pamoja na pia ni utekelezaji wa sera ya michezo ya kitaifa na michezo ipo ndani ya ratiba ya chuo, hivyo wafanyakazi mnapaswa kushiriki wote”. alisema.

 Aidha, Makamu mkuu wa chuo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo aligawa medali kwa washindi wa mbio za kilometa 5 na 10, Manahodha wa timu zilizoshiriki na wadau wa sekta ya michezo.

 Nayo, Idara ya michezo ya Chuo Kikuu Mzumbe, imewapongeza washiriki na wadau wa michezo kwa kufika katika bonanza hilo na kushukuru  menejimenti ya Chuo kwa kufanikisha bonanza hilo.

 Bonanza hilo lilihusisha wadau mbalimbali wa michezo ikiwemo wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe, timu alikwa  kutoka Mzinga, Kituo cha polisi Mzumbe, Moro ladies na Young warrious wa  Bwalo la umwema ambapo michezo mbalimbali ilichezwa ikiwemo  mpira wa miguu, mbio za kilomita 5 na 10,  mpira wa kikapu, mpira wa pete, mchezo wa bao na mchezo wa kusukuma kete.

                         ***************************************************************************

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka akiongoza mazoezi ya kunyoosha Viungo kwa wafanyakazi wa Chuo kikuu Mzumbe, Kulia  ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo (Taaluma) Prof. William Mwegoha

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Prof. Lughano akitoa zawadi za medali kwa washindi  na wadau mbalimbali katika viwanja vya Chuo, kampasi kuu Morogoro

 

Michezo mbalimbali iliyochezwa katika bonanza la chuo lilifonyika katika viwanja vya Chuo kikuu Mzumbe mwishoni wa wiki.

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka akiwa na wachezaji wa timu za kikapu, timu ya wanawake ya Mzumbe na timu ya Moro ladies.

Mzumbe University,
P.O Box 1 Mzumbe,
Morogoro, Tanzania.
Tel: 255 (0) 23 2931220/1/2
Fax: 255 (0) 23 2931216
Cell: 255 (0) 754694029
Email: .
Go to top